MPENDA PESA ELIUD OWALO ATUACHE TUPUMUE

Mkora Eliud Owalo

Kwa muda sasa tumekuwa tukishuhudia mijadala ya dhana bandia kutoka kwa Eliud Owalo, msaliti ambaye mafanikio yake yanaweza tu yakalinganishwa na fedha alizokusanya kutoka kwa Ruto mwaka 2013 baada ya kufichua mikakati ya muungano wa CORD.

Mtu aliyesaliti ndoto ya wakenya kwa kuuza siri za kampeni mwaka 2013 hatawafaa wakazi wa Kibra ambao waliathiriwa pakubwa na ulafi wa Owalo. Mbali na tetesi kutoka kwa wanaomchukia Raila, Owalo ni mtu anayeeneza nadharia na ambaye madai kuhusu tajiriba yake hayafai kutajwa kwa njia yoyote ile. Nani amesema kuwa mtu anahitaji tajiriba potovu aliyonayo Owalo kuwa kiongozi bora?

Baada ya kuhama chama cha ODM Zaidi ya mara kumi, tunamshukuru mungu hatimaye Owalo alihama chama hiki. Kibra si eneo la kutatua majungu ya kisiasa. Owalo alipewa na ODM jukumu la usimamizi wa kampeni za CORD lakini alivutiwa na mali haramu ya Ruto, akajiunga naye, ndiposa alifutwa kazi.
Inasikitisha kuwa maajenti wa CORD kwenye uchaguzi wa urais wa mwaka 2013 bado hawajalipwa mishahara yao licha ya kwamba Owalo alikabidhiwa mamilioni ya pesa kwa shughuli hiyo.

Owalo ni mporaji. Na kama alifuja fedha za maajenti wa CORD, kipi kitakachomzuia kuendelea na ulafi wake? Kama anajali maslahi ya maskini kama anavyodai, kwa nini alifuja fedha za kuajiri na kuwalipa maajenti hao?

Wafuasi wa ODM mtaani Kibra wanaweza kusahau kila kitu kingine lakini hawawezi kumsahau mtu katili kama Owalo, kikaragosi wa Ruto ambaye ameshawishiwa kuingia kwenye uchaguzi huu kugawanya kura za Waluo ili kuwezesha ushindi wa kikaragosi mwingine wa Ruto kwa jina Mariga. Mariga ambaye hana elimu ya kutosha anadhani ili mtu aisaidie jamii, lazima jamii impe kazi kwanza. Hii ni sababu ya kipumbavu ya kutaka uongozi.

Uchaguzi mdogo wa Kibra unajiri wakati ambapo walaghai wengi waliodai kuwa viongozi kwenye uchaguzi uliopita wamekuwa wakishughulika kwenye afisi zao kupora badala ya kutimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni. Walaghai maarufu kama Owalo lazima waaibishwe hadi wakati ule watakapojitokeza kueleza kwa nini walichagua pesa na kuwatenga wachochole ambao wanazidi kudidimia kwenye umaskini.

Would you like to get published on this blog? Email us on 254habari@gmail.com if you have any breaking news, Exposes, story ideas, human interest articles or interesting videos

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here